VINARA Barcelona watalazimika kusubiri
kwa wiki nyingine kushangilia taji la La Liga baada ya Cristiano Ronaldo
kufunga mabao mawili katika ushindi wa Real Madrid inayoshika nafasi ya
pili wa mabao 4-3 wakitokea nyuma dhidi ya Real Valladolid jana.
Kama Real isingeshinda, ushindi wa Barca
dhidi ya Real Betis Uwanja wa Nou Camp Jumapili ungewahakikishia taji
la nne ndani ya miaka mitano, wakiwa kileleni kwa pointi 13 zaidi zikiwa
zimebaki mechi nne zenye wastani wa pointi 12.
Valladolid, ambayo haijachukua pointi
Bernabeu kwa zaidi ya muongo, ilipata bao la kuongoza dakika ya nane
wakati Oscar Gonzalez alipomtungua kipa wa Real, Diego Lopez.
Mvunjaji rekodi: Cristiano Ronaldo amefunga mabao mawili na kufikisha mabao 199 Real Madrid
Nguvu: Ronaldo akienda hewani kuipiga kichwa cha nguvu kumtungua kipa wa Valladolid
WAFUNGAJI BORA LA LIGA
44 Lionel Messi (Barcelona)
33 Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
26 Radamel Falcao (Atletico Madrid)
19 Alvaro Negredo (Sevilla)
Roberto Soldado (Valencia)
16 Ruben Castro (Real Betis)
15 Piti (Rayo Vallecano)
Real ilisawazisha dakika ya 26 wakati
Marc Valiente alipobabatiza shiti la Angel Di Maria na kujifunga, kabla
ya Ronaldo kufunga bao lake la kwanza jana kwa kichwa dakika sita
baadaye.
Valladolid ilifunga kupitia kwa Javi Guerra dakika ya 35 na Kaka akaisawazishia tena Real dakika nne baadaye.
Ronaldo alifunga tena dakika 20 kabla ya
mchezo kumalizika akiunganishwa kwa kichwa kona, hilo likiwa nao la 33
kwa Mreno huyo katika msimu huu wa ligi.
Maumivu: Ronaldo kuna wakati aliumia jana
No comments:
Post a Comment