Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni
nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki
umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki.
Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na
kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na
kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao
vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto
baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo
yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila
mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo
ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku
survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani
mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani
asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho
na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe,
ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha
kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa,
Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua
wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu
alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka
jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja
wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza
mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua
kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu
wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo
yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa
Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha,
Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema
mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela
irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe
liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi,
hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina
Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme
majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake
ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE
No comments:
Post a Comment