Wednesday, April 24, 2013

VURUGU KUBWA CHUO CHA UHASIBU:....MKUU WA MKOA APIGWA MAWE, GODBLESS LEMA AFICHWA..!!


Vurugu  kubwa  zimeibuka  chuo  cha  uhasibu cha Arusha   baada ya mwanachuo kuchomwa kisu na mwanaakijiji na kufariki dunia....

Baada  ya  tukio  hilo, wanafunzi  walitoa  taarifa  kwa  mkuu wa chuo lakini  hakuwapa msaada wowote.


Walipokosa  msaada,wanafunzi  hao walianza  kuandamana  na taarifa zikafikishwa kwa mbunge  Godbless  lema ....


Mbunge  huyo  bila   hiyana akawasili na kufanikiwa kuwatuliza wanachuo hao maana nyumbani kwa Godbless  lema si mbali na chuo hicho ...

Baada  ya  taarifa  kumfikia Mkuu wa mkoa, ilimbidi  aliwasili na kuanza kuzungumza na wanachuo lakini baada ya kugundua uwepo wa Lema alianza kuongea  kwa  lugha  mbovu  na  ndipo wanachuo walipo kasirika na kuanza kumpiga mawe.


Hali  ilipochafuka,FFU  waliingia kazi  ya  kutuliza  ghasia...Hali ni mbaya sana lakini cha kushangaza askari mmoja aliwatonya wanachuo wamfiche Lema


Godbless  Lema  anasakwa mpaka sasana  hajulikani alipo baada ya wanachuo kumficha kusiko julikana.








No comments:

Post a Comment