Saturday, June 8, 2013

KALA JEREMIAH NA OMMMY DIMPOZ WATISHA


Mwaka huu umekuwa mwaka mzuri zaidi kimuziki kwa msanii toka rock City Mwanza Kala Jeremiaha ambae maombi yake kwa ‘Dear God’ yamesikika na amepata majibu kwa njia ya kipekee na wimbo wake ‘Dear God’ umeweza kuchukua tuzo tatu katika Kilimanjaro Music Awards 2013.  
 
Kala Jeremiah ametumia mkuki mmoja kunasa ‘swala’ wake watatu muhimu mwaka huu, Dear God imeweza kumpa nafasi kubwa na kushinda tuzo katika kipengele cha wimbo bora wa Hip Hop.



Nguvu ya wimbo huo hapana shaka ndiyo imemuwezesha pia kuondoka na tuzo ya msanii bora wa Hip Hop na Mtunzi bora wa mashairi ya Hip Hop.

Kala aliweza kuwapenya wasanii wazito kama Fid Q, Joh Makini, Mwana FA, Profesa Jay na mdogo wake katika game Stamina wa Moro Town waliokutana nae katika vipengele vya Hip Hop.

Wimbo huu ulitengenezwa na mtayarishaji chipukizi Dee Classic ambae pia alikuwa anawania tuzo katika kipengele cha mtayarishaji chipukizi wa Mwaka lakini hakuweza kushinda tuzo hiyo ambayo ilienda kwa Mesen Selector.

Msanii mwingine wa bongo fleva aliyeng’ara katika tuzo hizo ni Ommy Dimpoz ambae pia aliondoka na Tuzo tatu, ambazo ni Video bora ya wimbo bora ya mwaka, wimbo bora wa Bongo Pop ‘Me and You’ akiwa na Vannessa Mdee ambao pia uliwapa tuzo ya wimbo bora wa kushirikishwa/kushirikiana.

Wasanii na watayarishaji wa muziki wa bongo fleva ambao kwa mara ya kwanza wameweza kujishindia tuzo za Kili ni pamoja na kundi la Jambo Squared toka Arusha (Kundi bora la muziki wa kizazi kipya), Rama Dee ‘Kinega’ (Wimbo bora wa RnB ‘Kuwa na subira).

Wengine ni Amini (Wimbo bora wa Zouk Rhumba ‘Ni wewe’), Recho (Msanii bora wa kike Bongo fleva), na Nay wa Mitego (Wimbo bora wa Hip Hop ‘Nasema Nao’). Mesen Selecter (Mtayarishaji chipukizi wa Mwaka), Ali Nipishe (Msanii bora anaechipukia).

Tuzo hizo zimeshuhudiwa huku mfalme na malkia wa muziki wa kibongo wakitangazwa kuwa Lady Jay Dee ‘Anaconda’ (Msanii bora wa Kike) na Diamond Platinumz (Msanii bora wa kiume).

Friday, June 7, 2013

MWANAUME AFARIKI DUNIA NDANI YA URODA GEST HOUSE ILIYOKO MANZENSE LEO MCHANA......


Difenda  ya  polisi  ikiuchukua  mwili  wa  marehemu...

Mwanaume mmoja ambaye hakujulikana jina lake leo amekutwa amekufa katika gesti bubu iitwayo Uroda iliyopo Manzese Midizini jijini Dar. 


Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio ni kwamba marehemu alikuwa na mpenzi wake ambaye waliingia wote katika gesti hiyo lakini alikutwa jamaa peke yake.

 Mwili wa marehemu umepelekwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

Thursday, June 6, 2013

HATIMAYE NGWEA AZIKWA KWENYE MAKABURI YA KIBONDA MKOANI MOROGORO

Baada ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair leo amezikwa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao.

Kabla ya kuzikwa, wananchi wa Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili wake kwenye uwanja wa Jamhuri.

 
 Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini Afrika Kusini, wiki iliyopita. Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao wamehudhuria mazishi hayo.
16f11344cea711e2813a22000a1f8f34_7
75e8603ecea511e29ecd22000aaa08de_7
4406673ccea511e2850422000a1f9a85_7
“Marehemu Albert Mangweha azikwa kishujaa sana ni umati usioelezeka mungu akulaze mahali pema peponi,” ameandika Izzo B kwenye Instagram.


Naye Lady Jaydee kupitia Twitter ameandika: Mpk hapa tulipomsindikiza panatosha. Mungu amrehemu, kazi tumeimaliza. Life goes on.”
e1147594cea211e2a86422000a1f9839_7
ee9d94facea411e2a9ea22000ae81462_7
f18745b2cea411e2aa3022000a9e2931_7